• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapongezwa kwa juhudi zake katika kuhimiza ushirikiano wa kimataifa wa kuthibiti kuenea kwa jangwa

    (GMT+08:00) 2017-06-21 17:57:30

    Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi na mwenzi wake wa Kenya Bw. Macharia Kamau wakiwa ni wenyekiti wa pamoja wa kikundi cha "marafiki wa dunia isiyo na uchafuzi", wameongoza mkutano wa kazi ya kuzuia kuenea kwa jangwa uliofanyika mjini New York, Marekani.

    Kwenye mkutano huo, wajumbe wa kudumu wa nchi mbalimbali katika Umoja wa Mataifa wameipongeza China kwa juhudi za kuhimiza ushirikiano wa kimataifa katika kuzuia kuenea kwa jangwa, na kusema miradi ya ushirikiano kati ya China na nchi zinazoendelea imezisaidia nchi hizo kuimarisha uwezo wa kuzuia ardhi isibadilike kuwa jangwa, kuinua usalama wa chakula na kuboresha mazingira ya kiasili.

    Pande mbalimbali zimekubali kuhudhuria mkutano wa 13 wa nchi zilizosaini makubaliano ya kuzuia kuenea kwa jangwa wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika mwezi Septemba mwaka huu hapa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako