• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfalme wa Saudia amtaja mwanawe kama mrithi wa mfalme akichukua nafasi ya Nayef

    (GMT+08:00) 2017-06-21 18:59:24

    Mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud ametangaza kuwa mtoto wake mwanamfalme Mohammed bin Salman kuwa mrithi wa mfalme wa nchi hiyo, akichukua nafasi ya mwanamfalme Mohammed bin Nayef.

    Kufuatia amri ya Mfalme iliyotolewa na Shirika la Habari la Saudia, aliyekuwa mrithi wa mfalme pia ataondolewa kwenye wadhifa wake kama waziri wa mambo ya ndani, huku mwanamfalme Salman akiteuliwa kuwa naibu waziri mkuu, na pia anaendelea na wadhifa wake wa waziri wa ulinzi.

    Shirika hilo limethibitisha kuwa wajumbe 31 kati ya 34 wa Baraza la Utii la Saudia walimchagua Mohamed bin Salman kuwa mrithi wa mfalme.

    Hakuna sababu iliyotolewa kwa mabadiliko hayo ya ghafla.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako