• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wadau wa kilimo Tanzania wapongeza serikali kwa kufuta uagizaji wa sukari kutoka nje

    (GMT+08:00) 2017-06-21 19:10:10

    Wadau wa kilimo cha miwa nchini Tanzania wamesema hatua ya serikali kupiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje imepelekea viwanda vya sukari kuwalipa wakulima wa miwa bei ya juu.Kwa mujibu wa kiongozi wa timu ya wakulima wa miwa Bw Job Zahoro, kumekuwa na ongezeko la malipo kwa jumla tangu kiwanda cha sukari cha Kilombero kianzishwe kianzishwe mwaka wa 1999. Ameongeza kuwa kiwanda hicho kiliwalipa wakulima wadogo wadogo jumla ya shilingi bilioni moja ukiondoa mshahara lakini kwa msimu ulioisha kimelipa jumla ya shilingi bilioni 47 ambazo zinasaidia kuboresha maisha ya wakulima katika eneo ambako kiwanda hicho kipo. Taarifa hiyo inakuja miezi michache tu baada ya rais John Pombe Magufuli kupiga marufuku uagizaji wa sukari kutoka nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako