• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukame unaoikabili Kenya unaweza kuathiri usafirishaji wa mboga

    (GMT+08:00) 2017-06-22 09:35:21

    Mwenyekiti wa jumuiya ya wauzaji wa vyakula freshi ya Kenya Bw Apollo Owour amesema ukame ulioikabili Kenya mapema mwaka huu unaweza kuathiri usafirishaji nje wa mboga kwa mwaka huu.

    Akiongea kwenye mkutano mjini Nairobi Bw Owour amesema usafirishaji wa vyakula hivyo huwa unaathiriwa na ukame, lakini kama kukiwa na mvua ya kutosha hali inaweza kubadilika, kwa kuwa inahitaji miezi mitatu tu kwa bidhaa za mboga kukomaa.

    Mwaka jana Kenya ilisafirisha nje tani elfu 56.6 za mboga, kati ya hizo maharage mabichi yalichukua asilimia 60 na maparachichi yalichukua asilimia 15.

    Sehemu kubwa ya bidhaa hizo huuzwa kwenye soko la Umoja wa Ulaya, na sehemu kubwa inauzwa Uingereza. Soko hilo lina hatari hasa baada ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako