• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo kati ya China na Marekani kuhusu masuala ya diplomasia na usalama yaanza Washington

    (GMT+08:00) 2017-06-22 09:50:55
    Mazungumzo ya duru ya kwanza kati ya China na Marekani kuhusu mambo ya diplomasia na usalama yameanza jana mjini Washington.

    Katika mazungumzo hayo, China na Marekani zitabadilishana maoni juu ya uhusiano wa pande mbili na masuala muhimu ya kimataifa na kikanda.

    Mazungumzo hayo yamefanyika kutokana na makubaliano yaliyofikiwa na rais Xi Jinping wa China na mwenzake wa Marekani Donald Trump walipokutana Mar-a-Lago huko Florida. Mjumbe wa taifa wa China Bw Yang Jiechi na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw Rex Tillerson na waziri wa ulinzi wa Marekani Bw James Matisse wameendesha mazungumzo hayo kwa pamoja.

    Utaratibu wa mazungumzo kati ya China na Marekani ni nguzo muhimu ya kuendeleza uhusiano wa pande mbili. Kabla ya hapo, serikali za nchi mbili zimeahidi kufanya juhudi kwa pamoja ili kufanikisha mazungumzo hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako