• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri wa mambo ya nje wa China ahudhuria mazungumzo kati ya China na Afrika kuhusu kupunguza umaskini

    (GMT+08:00) 2017-06-22 09:51:03

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi jana huko Addis Ababa alihudhuria ufunguzi wa mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu upunguzaji wa umaskini na Baraza la jumuiya ya washauri bingwa kati ya China na Afrika, na kutoa hotuba kuhusu ushirikiano kwenye kuondoa umaskini.

    Bw. Wang Yi pia amefanya mazungumzo na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat, na kusema China inapenda kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Afrika.

    Bw. Wang Yi ameutaja umaskini kuwa ni adui wa binadamu wote na chanzo cha migogoro na ugaidi, na kusema nchi za Afrika zinaweza kuiga uzoefu wa China katika kuondoa umaskini.

    Pia amesema China inapenda kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika katika utawala wa taifa, kupunguza umaskini, kutoa mafunzo ya ujuzi, usalama wa chakula, miundo mbinu, na afya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako