• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Malkia wa Uingereza atoa mwito wa kuhakikisha utulivu baada ya Brexit

    (GMT+08:00) 2017-06-22 09:51:31

    Malkia Elizabeth II wa Uingereza ametangaza kwamba atadumisha utulivu wa taifa na kuhakikisha nchi yake inajitoa kutoka kwenye Umoja wa Ulaya kwa utaratibu.

    Malkia Elizabeth II amesema hayo jana alipohutubia ufunguzi wa bunge jipya la Uingereza, na kutangaza mipango ya utawala kwa miaka miwili ijayo.

    Amesema kufikia makubaliano mazuri na Umoja wa Ulaya kutakuwa ni kazi muhimu kwa serikali ya Uingereza. Kati ya mipango mipya 27 ya serikali aliyotangaza siku hiyo, kuna mipango 8 inayohusu kujitoa Umoja wa Ulaya, ikiwemo mipango ya sheria, ushuru na uhamiaji.

    Ameongeza kwamba serikali ya Uingereza itatafakari sera zake za sasa na kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi kupitia utungaji wa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako