• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wapiganaji wa kundi la IS walipua msikiti maarufu wa al-Nuri huko Mosul

    (GMT+08:00) 2017-06-22 10:07:07

    Jeshi la Iraq limesema, wapiganaji wa kundi la IS wamelipua msikiti wa kihistoria wa al-Nuri, wakati jeshi hilo likisonga karibu na eneo la msikiti huo magharibi mwa Mosul.

    Kituo cha operesheni ya pamoja kimetoa taarifa ikisema, wapiganaji hao walilipua msikiti huo na mnara wake vilivyoko umbali wa mita 50 kutoka msikiti ulioko katikati ya mji mkongwe, magharibi mwa Mosul.

    Msikiti huo maarufu na mnara wake ambao umeupatia mji huo jina la "al-Hadbaa" ni mahali ambapo mwezi wa Juali mwaka 2014, kiongozi wa kundi la Is Bw Abu Bakr al-Baghadadi alitangaza kuanzishwa kwa milki ya khalifa nchini Iraq na Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako