• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo kuhusu maendeleo na kupunguza umaskini barani Afrika na Mkutano wa jopo la washauri bingwa wa China na Afrika wafunguliwa Ethiopia

    (GMT+08:00) 2017-06-22 18:37:10

    Mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu maendeleo na kupunguza umaskini barani Afrika, na Mkutano wa jopo la washauri bingwa wa China na Afrika yamefunguliwa jana katika kituo cha mkutano cha Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Waziri wa mambo ya nje wa China Bw Wang Yi na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw Moussa Mahamat wamehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa mkutano huo.

    Bw Wang Yi ametoa hotuba akisema watu milioni 400 wa Afrika wanaishi katika umaskini, na Wachina zaidi ya milioni 40 wanahitaji kuondokana na umaskini. Ni wajibu wa China kushirikiana katika kupambana na umaskini na kupata maendeleo ya pamoja, ambalo ni lengo la pamoja, na ni mahitaji ya maendeleo ya kijamii.

    Amesema, "China inapenda kuzidisha mawasiliano na nchi za Afrika kuhusu uzoefu wa kutawala nchi, kutafuta njia ya maendeleo na kupunguza umaskini kwa kufuatana na mahitaji ya nchi za Afrika. China inapenda kubadilishana uzoefu na marafiki zetu za Afrika."

    Bw Moussa Faki Mahamat amesema anapenda ushirikiano wa pande mbili katika kupunguza umaskini upate mafanikio.  

    Amesema, "Uhusiano kati ya China na Afrika umepata maendeleo makubwa chini ya msingi wa usawa, kuaminiana, kuheshimiana na kunufaishana. Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika limehimiza ushirikiano wa pande mbili upate mafanikio makubwa. Kitu ambacho Afrika imejifunza ni kwamba China imefanya juhudi nyingi za kujitegemea na kuondokana na umaskini."

    Katika mkutano huo, wataalamu na wasomi wa Afrika wameona kwamba migogoro na vita ni sababu kubwa zinazosababisha umaskini barani Afrika. Naibu mkuu wa Chuo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Cameroon Bw Stephane Ngwanza amesema mfumo wa kisiasa wenye utulivu unafanya kazi kubwa katika kuendeleza uchumi na kuondokana na umaskini.

    Amesema, "Hali ya utulivu wa kisiasa imeisaidia China kupata maendeleo. Lakini kwa upande wa Afrika, migogoro na vita vinaifanya hali ya umaskini iwe mbaya. Afrika iliwahi kutawaliwa na nchi za kigeni, na kuharibu heshima yake. Zaidi ya hayo, vita ya wenyewe kwa wenyewe pia imezuia maendeleo ya nchi husika za Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako