• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania ataka kuvutia uwekezaji zaidi wa China

    (GMT+08:00) 2017-06-22 20:06:30

    Rais John Magufuli wa Tanzania ameeleza matumaini ya kuvutia zaidi uwekezaji wa China, na kusukuma mbele uhusiano kati ya nchi hizo mbili bila kusita.

    Rais Magufuli amesema hayo jana aliposhiriki kwenye hafla ya kuzinduliwa kwa kiwanda cha chuma cha Kiluwa kilichowekezwa na China. Amesema uwekezaji kama huo ni muhimu sana kwa Tanzania kutimiza utandawazi wa viwanda. Amezikaribisha kampuni za China kuwekeza zaidi nchini Tanzania, na kuisaidia nchi hiyo kupata maendeleo kwa pande zote.

    Kwa upande wake, balozi wa China nchini Tanzania Bw. Lv Youqing ambaye alihudhuria hafla hiyo, amezitaka kampuni za China zifanye juhudi kutekeleza majukumu ya jamii, na kutoa mchango kwa maendeleo ya uchumi nchini Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako