• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Barclays Kenya kuwaachisha kazi wafanyakazi 300

    (GMT+08:00) 2017-06-22 20:17:51

    Benki ya Barclays nchini Kenya inapanga kuwaachisha kazi wafanyakazi 300 ikiwa ni mojawepo wa mipango yake ya kukata gharama za oparesheni.

    Hata hivyo kwenye taarifa benki hiyo imesema kuna chaguo la wale wanaotaka kuacha kazi kwa hiari na kwamba kupitia kwa mpango huo hatimaye itahitaji kuwaachisha watu 130 kazi moja kwa moja.

    Barclay inatarajia kuendea na mpango wake huo wa upunguzaji kwa mwezi mmoja ukiwa ulianzia Juni 19.

    Barclays inajiunga na orodha ya benki kadhaa ambazo zimetangaza kupunguza wafanya kazi wake na pia kufunga baadhi ya matawi.

    Benki tisa hizi zikiwemo zile za serikali KCB na National Bank tayari zimetangaza mipango ya kupunguza waajiri wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako