• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Ujenzi wa barabara ya Jomvu - Mombasa kuanza

    (GMT+08:00) 2017-06-22 20:18:06

    Ujenzi wa barabara kuu ya kutoka eneo la Jomvu hadi Mjini Mombasa nchini Kenya unatarajiwa kuanza baada ya kandarasi ya shilingi bilioni 6.5 kutolewa.

    Mkurungezi wa mamlaka ya ujenzi wa barabara nchini Kenya Peter Mundinia amesema kandarasi hiyo imepewa kampuni ya China Engineering kujenga barabara hiyo ia kilomita 10 ndani ya miezi 30.

    Baada ya kukamilika sasa barabara hiyo itapanuka na kuwa ya laini sita na hivyo kupunguza msongamano unaotatiza usafiri eneo hilo na pia uchukuzi wa shehena kutoka bandari ya Mombasa.

    Mundinia alisema hayo wakati wa ukaguzi wa barabara ya kilomita 41 ya Mombasa hadi Mariakani inayojengwa kwa ufadhili wa benki ya maendeleo ya Afrika AfDB.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako