• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wachimbaji Bauxite Msitu wa Shengena Tanzania watakiwa kufuata taratibu.

    (GMT+08:00) 2017-06-22 20:19:20

    Watu Wanaofanya uchimbaji Msitu wa Shengena nchini Tanzania wametakiwa kufuata taratibu.

    Mbunge wa Same Mashariki Naghenjwa Kaboyoka amesema kuna athari za kimazingira zinazotokana na uchimbaji wa madini ya Bauxite katika Msitu huo

    Akijibu swali hilo bungeni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani, amesema kuwa mtu au taasisi itakayohitaji kufanya shughuli za uchimbaji ndani ya hifadhi hiyo atatakiwa kufuata taratibu za kisheria.

    Amesema taratibu hizo ni zile zitakazozingatia masuala muhimu ikiwamo kufanyika kwa Tathmini ya Athari za Mazingira (TAM) kabla ya kuanza kwa uchimbaji.

    Hata hivyo amesema hadi sasa hakuna taarifa rasmi kuhusu uchimbaji wa madini ya Bauxite katika Hifadhi ya Shengena.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako