• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania aamuru viwanda vilivyobinafsishwa na kulala vichukuliwe na serikali

    (GMT+08:00) 2017-06-23 09:09:24

    Rais John Magufuli wa Tanzania ametoa amri ya kuchukuliwa kwa viwanda vya serikali vilivyouzwa kwa wawekezaji binafsi ambao wameshindwa kuviendeleza.

    Rais Magufuli amemwamuru waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Bw Charles Mwijage, kutwaa viwanda hivyo na kuwapatia wawekezaji makini.

    Akiongea baada ya ziara ya siku tatu katika mkoa wa pwani, Rais Magufuli amesema serikali iliamua kuuza viwanda 197 kwa wawekezaji binafsi kwa lengo la kutaka viendelezwe, lakini vingi vimelala na baadhi matumizi yake yamebadilishwa.

    Uamuzi wa Rais Magufuli unaendana na ahadi aliyotoa kwenye kampeni mwaka 2015, kuwa serikali yake haitasita kutwaa viwanda vilivyolala na kuwapatia wawekezaji makini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako