• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama cha ANC chasema kura ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma itashindwa

    (GMT+08:00) 2017-06-23 09:09:43

    Chama tawala cha Afrika Kusini ANC kimesema kura yoyote ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini itashindwa.

    Jana mahakama ya katiba ya Afrika Kusini ilitoa uamuzi kuwa spika wa bunge la Afrika Kusini Bibi Beleka Mbete ana madaraka ya kuamua kama kura za kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma zinaweza kupigwa kwa siri.

    Taarifa iliyotolewa na ANC inasema bila kujali kama ni kura siri au hapana, kama ilivyokuwa mara kadhaa huko nyuma, upigaji kura huo utashindwa. Mpaka sasa Rais Zuma amenusurika kura hiyo mara saba.

    Mwezi Aprili Chama cha upinzani cha UDM kiliiomba mahakama iamuru uamuzi wa kura ya siri, ili kutoa nafasi kwa wabunge wa chama cha ANC kupiga kura dhidi ya Rais Zuma.

    Msemaji wa ANC Zizi Kodwa amesema chama chake kinakaribisha uamuzi wa mahakama, na kinaamini kuwa spika wa bunge atatumia busara zake kabla ya kufanya uamuzi, na uamuzi wake utaheshimiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako