• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa wazindua mpango mpya wa kuhimiza maendeleo ya Kenya

    (GMT+08:00) 2017-06-23 09:17:41

    Umoja wa Mataifa umezindua mpango mpya wa kuhimiza juhudi za Kenya kupata maendeleo shirikishi kwa kulingana na ruwaza ya nchi hiyo 2030.

    Mpango wa msaada wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa UNDAF wa mwaka 2018-2022 pia utasaidia kuhimiza uungaji mkono kutoka kwa nchi wahisani, sekta binafsi na jumuiya zisizo za kiserikali.

    Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Kenya Siddharth Chatterjee amesema, mpango huo ni njia yenye uvumbuzi ya kupata maendeleo ambao utaiwezesha Kenya kutatua suala la umaskini. Ameongeza kuwa, mpango huo unaonyesha sekta zinazopewa kipaumbele kuendelezwa, ili kuhakikisha Kenya inatimiza ruwaza yake ya kuwa nchi yenye mapato ya kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako