• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya waamua kuimarisha mabadilishano ya habari mipakani na mapambano dhidi ya ugaidi kwenye mtandao wa Internet

    (GMT+08:00) 2017-06-23 09:35:47

    Mwenyekiti wa Kamati ya Ulaya Bw. Donald Tusk‎ amesema, viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya wamefikia makubaliano kuhusu kuimarisha mabadilishano ya habari mipakani na mapambano dhidi ya ugaidi kwenye mtandao wa Internet katika mkutano wa wakuu wa umoja huo.

    Bw. Tusk amesema, ugaidi bado ni tishio kubwa linaloikabili Ulaya. Nchi wanachama wa umoja huo wamekubaliana kuhimiza mabadilishano ya habari mpakani, ili kuwazuia magaidi wa Mashariki ya Kati wasirudi barani Ulaya.

    Habari nyingine zinasema waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amewaambia viongozi wa Umoja wa Ulaya kwamba raia wa umoja huo wanaoishi nchini Uingereza kwa miaka mitano watapewa hadhi ya "wakazi wa EU".

    Hadhi hiyo mpya ya uhamiaji itahakikisha haki zao za kukaa nchini Uingereza na kupata huduma mbalimbali ikiwemo afya na elimu baada ya nchi hiyo kujitoa umoja huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako