• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kocha wa Kenya ataja kikosi cha wachezaji 15 wa raga kila upande

    (GMT+08:00) 2017-06-23 09:57:29

    Kocha Jerome Paarwater ametaja kikosi cha Kenya cha wachezaji 15 kila upande kitakachomenyana na Uganda katika mechi ya ufunguzi ya Kombe la Dhahabu la Afrika (Africa Gold Cup) uwanjani RFUEA jijini Nairobi, Jumamosi.

    Paarwater ameweka imani yake kwa wachezaji 20 waliotesa Kampala Uganda mnamo Juni 10 na kuita wachezaji watatu wapya Kenny Andola (KCB), Brad Owako (Mwamba) na chipukizi matata Steve Otieno (Homeboyz).

    Kenya Simbas iliilemea Uganda pointi 23-18 jijini Kampala baada ya kutoka nyuma wakiwa na 10-18 katika mechi ya mkondo wa kwanza ya Elgon Cup. Mechi ya kesho itakuwa ya marudiano ya Elgon Cup. Mshindi kwa jumla ya pointi baada ya mikondo miwili atatawazwa bingwa wa Elgon Cup. Uganda, ambayo ilipepetwa 48-10 jijini Kampala na 45-24 jijini Nairobi ilipokutana na Kenya mwaka 2016, ilitangaza kikosi chake Jumatano. Mbali na Uganda, Kombe la Dhahabu la Afrika pia linajumuisha Namibia, Zimbabwe, Senegal na Tunisia. Timu nne-bora katika mashindano haya ya mataifa sita zitafuzu kushiriki Kombe la Dhahabu la Afrika mwaka 2018 ambalo litatumika kuchagua mwakilishi wa Afrika katika Kombe la Dunia mwaka 2019.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako