• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mohamed Salah kupokea donge nono zaidi Liverpool

    (GMT+08:00) 2017-06-23 09:57:52

    Baada ya kushindwa kutamba na klabu ya Chelsea ya England kama alivyokuwa akiichezea FC Basel ya Uswiss, Mohamed Salah alilazimika kukubali kutolewa kwa mkopo kwa kushinda kujihakikishia nafasi ya kudumu Stamford Bridge. Salah alitolewa kwa mkopo katika club za Fiorentina na AS Roma kabla ya mwaka 2016 AS Roma kuamua kumsajili kwa jumla. Hata hivyo jana Mohamed Salah alifanikiwa kurudi England kwa kusajiliwa na Liverpool akitokea AS Roma kwa dau la pound milioni 39.

    Usajili wa winga huyu umevunja rekodi ya usajili kwa wachezaji waliowahi sajiliwa na timu hiyo ambapo usajili wa gharama zaidi ulikuwa wa mshambuliaji Andy Carrol, aliposajiliwa kwa dau la pauni milioni 35 mwaka 2011.

    Salah raia wa Misri mwenye umri wa miaka 25 amesaini mkataba wa miaka mitano kuweza kutumikia Liverpool.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako