• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tetesi za usajili katika bara la Ulaya

    (GMT+08:00) 2017-06-23 09:58:53

    Katika dirisha hili la usajili, klabu ya Portsmouth imetangaza kumsajili beki Nathan Thompson kwa mkataba wa miaka miwli. Na kiungo wa klabu ya Gillingham, Elliot List amekubali kuongeza mkataba wa mwaka mmoja ndani ya klabu hiyo, kwa mkataba huo utamfanya adumu mpaka mwisho wa msimu wa mwaka 2017/18. Mchezaji wa klabu ya Chelsea, Diego Costa amesema anahitaji kusaini kwa miamba ya Hispania timu ya Atletico Madri, mchezaji huyo aliondoka Atletico mwaka 2014.

    Chelsea nao wamepiga hodi katika ligi ya Serie kujaribu kutafuta mlinzi atakayeimarisha ngome yao ya ulinzi.

    Taarifa zinasema raisi wa klabu ya Juventus Beppe Marotta amesema wamepokea ofa nzuri kutoka klabu ya Chelsea kwa mlinzi wao Alex Sandro, japokuwa hakuna taarifa rasmi kuhusu kiasi kilichotumwa na Chelsea lakini inasemekana ni zaidi ya euro 70m.

    Klabu ya Manchester United imefikia makubaliano na klabu ya Real Socieadad kumuuza winga wao Adnan Januzaj ambaye anatarajia kujiunga na Wahispania hao kwa dau la euro 9.7m. Aidha mshauri wa mshambuliaji Cristiano Ronaldo amesema hakuna klabu Uingereza inayoweza kumchukua Ronaldo zaidi ya Manchester United kwani hapo ndipo Ronaldo anapopawaza zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako