• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Askari polisi watano wauawa kwenye mlipuko uliotokea kusini magharibi mwa Pakistan

    (GMT+08:00) 2017-06-23 16:47:25

    Watu 11 wameuawa wakiwemo askari polisi watano na wengine 16 kujeruhiwa katika shambulizi la kujitoa muhanga lililotokea kwenye kituo cha ukaguzi mjini Quetta, kusini magharibi mwa Pakistan leo.

    Msemaji wa Hospitali ya Quetta amesema huenda idadi ya vifo ikaongezeka kwa sababu baadhi ya majeruhi wako kwenye hali mbaya.

    Naibu Inspekta wa polisi Abdul Razzaq Cheema amesema, tukio hilo limetokea majira ya saa tatu asubuhi kwa saa za huko, wakati mtu mmoja alipolipua gari lililotegwa mabomu katika kituo cha ukaguzi karibu na ofisi ya mkuu wa polisi iliyoko barabara ya Gulistan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako