• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya Afrika Mashariki yatoa thamani ya ushuru kwa Eneo la Biashara Huria ya Pande Tatu

    (GMT+08:00) 2017-06-23 16:52:40

    Kamati ya uwekezaji wa biashara, viwanda na fedha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imetoa rasmi thamani ya ushuru kwa Misri na Afrika Kusini katika siku za karibuni.

    Kitendo hicho kimeonyesha maendeleo muhimu katika mjadala wa Eneo la Biashara Huria ya Pande Tatu TFTA, na kuweka msingi katika kuhimiza kuidhinisha mkataba wa TFTA ndani ya mwaka huu.

    Viongozi kutoka nchi 26 za Afrika walihudhuria mkutano wa kilele wa uchumi wa Afrika uliofanyika mwezi Juni mwaka 2015 mjini Sharm e-Sheikh, Misri na kufikia makubaliano ya kusaini mkataba unaoyahusisha mashirika matatu ya kiuchumi ya Afrika ambayo ni Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika COMESA, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, na Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC. Pia mkataba huo unaelekeza kuanzisha Eneo la Biashara Huria ya Pande Tatu TFTA likiwa ni eneo kubwa kabisa la biashara huria barani Afrika.

    Baada ya TFTA kuzinduliwa rasmi, thamani ya jumla ya pato la taifa la nchi husika zenye watu milioni 625 imefikia dola bilioni 1,200 za kimarekani, ambayo imechukua asilimia 58 ya pato la jumla la Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako