• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe kuhamishia wanyamapori 2000 nchini Msumbiji

    (GMT+08:00) 2017-06-23 16:54:42

    Zimbabwe itawahamisha wanyamapori 2000 na kuwapeleka nchi jirani ya Msumbiji ili kupunguza idadi kubwa ya wanyamapori katika hifadhi za nchi hiyo.

    Msemaji wa idara ya usimamizi wa hifadhi ya taifa ya wanyamapori ya Zimbabwe Bw. Simukai Nyasha amesema wanyama watakaohamishwa ni pamoja na Nyumbu 300, Nyati 200, Tembo 50, Twiga 100, Pundamilia 200 na Swala zaidi ya 1000. Wanyama hao watapelekwa kwenye hifadhi ya kitaifa ya Zinave kusini magharibi mwa Msumbiji kutoka hifadhi ya Bonde la Save kusini mashariki mwa Zimbabwe.

    Msemaji huyu amesema kazi hiyo inalenga kuhakikisha kuwepo kwa aina mbalimali za viumbe katika hifadhi ya Bonde la Save, na kutatua ukosefu wa uwiano unaotokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wanyama wakubwa wanaokula majani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako