• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bunge la Somalia lapitisha muswada wa sheria wa marekebisho ya sekta ya mawasiliano ya simu

    (GMT+08:00) 2017-06-23 18:13:29

    Bunge la Somalia limepitisha kwa kauli moja muswada wa Sheria ya Taifa ya Mawasiliano ambao unatarajiwa kurekebisha sekta ya mawasiliano ya simu nchini humo.

    Muswada huo uliowasilishwa na waziri wa Posta, Simu na Teknolojia Abdi Ashur Hassan, ni moja ya miswada ya muda mrefu ambayo ilikuwa bado haijapitishwa na bunge. Waziri huyo amesema, mara baada ya muswada huo kusainiwa, utafanya marekebisho kwenye sekta ya mawasiliano ya simu, ambayo moja ya sekta zinazokua kwa kasi nchini Somalia, na kulinda haki za mtumiaji na mwekezaji.

    Waziri huyo amesema, muswada huo ulikuwa moja ya vipaumbele vya uongozi mpya wa wizara yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako