• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki kuu ya Kenya na chama cha Benki wazindua mtandao wa maelezo kwa wateja

    (GMT+08:00) 2017-06-23 19:44:51

    Benki kuu ya Kenya ikishirikiana na Chama cha benki nchini Kenya KBA wamezindua rasmi mtandao ambao utaonyesha gharama ya kukopesha pesa katika harakati walizotaja kuwa kuhimiza uwazi na ushindani katika sekta hiyo. Mtandao huo unatarajiwa kutoa maelezo kuhusiana na ada na malipo mbali mbali ya mikopo inayotolewa na benki na mashirika madogo ya kifedha nchini Kenya. Hatua hiyo inatarajiwa kuwasaidia wateja kuweza kufanya uamuzi kuhusiana na benkiwatakazotembelea kuomba mikopo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na benki hiyo, maelezo yatahusiana zaidi na mikopo ya kibinafsiyenye udhamini , isiyokuwa na udhamini na pia mikopo ya kununua nyumba.Hata hivyo taarifa hiyo imesema kuwa huduma nyingine zinazotolewa na benki hizo zitaendelea kujumuishwa polepole kwa mtandao huo. Wateja pia wanaweza kufikia mtandao kupitia simu zao pamoja na kudondosha utaratibu wa kulipa mkopo.Aidha taarifa hiyo pia imewatahadharisha wateja kuwa habari zilizopo kwa mtandao zinalenga kuongezea kwa zile zinazotolewa na benki zenyewe chini ya sheria ya mashirika madogo ya kifedha kuhusiana na ada zao kwa mikopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako