• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utafiti waonyesha fedha kwa serikali kuu zatolewa haraka kuliko za kaunti nchini Kenya

    (GMT+08:00) 2017-06-23 19:45:16

    Shirika la kimataifa linalojihusisha na mambo ya bajeti International Budget Partnership IBP limesema wizara ya fedha ya Kenya huchelewesha fedha za kufadhili serikali za kaunti ikilinganishwa na serikali kuu. Kwenye utafiti wake, IBP imesema katika utafiti wake wa miaka sita imegundua kuwa fedha za kufadhili serikali kuu uidhinishwa haraka zaidi kuliko za kaunti. Mkuu wa kitengo cha utafiti cha shirika hilo Bwana John Kinuthia amesema hatua hiyo huathiri pakubwa shughuli za serikali za kaunti. Ameitaka wizara ya fedha kuhakikisha fedha zinazotengewa serikali kuu na zile za kaunti zitolewa kwa wakati mmoja ili kuwezesha serikali za kaunti kutekeleza miradi yake ya maendeleo katika maeneo ya mashinani. Ameongeza kuwa mfumo wa ugatuzi utafaulu tu ikiwa fedha hizo zitatolewa kwa wakati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako