• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki ya dunia yapongeza juhudi za Tanzania katika kupambana na ufisadi

    (GMT+08:00) 2017-06-23 19:45:30

    Benki ya dunia imepongeza hatua zilizochukuliwa na Tanzania katika kupambana na rushwa nchini humo. Benki hiyo pia imetoa njia tano kwa Tanzania zitakazoongeza ufanisi kwenye vita hivyo badala ya kutegemea kuboresha sheria au kuwaanika hadharani watu waliohusika na ufisadi.Kwa mujibu wa mjumbe wa benki hiyo katika nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi Bwana Bella Bird, mafanikio katika vita dhidi ya rushwa ni muhimu kwa maendeleo ya nchi inayopambana na umaskini.Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 20 cha kupambana na rushwa cha benki hiyo wameshirikiana na nchi mbali mbali kupambana na rushwa na pia wamejifunza mengi ikiwemo haja ya serikali kuboresha motisha kwa wafanyakazi wake.Aidha Bwana Bird amesema Benki hiyo iko tayari kuisaidia Tanzania kupunguza ufisadi ili kuboresha utoaji wa huduma bora zitakazong'arisha maisha ya wananchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako