• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping asisitiza kutafuta njia ya kuondoa umaskini katika sehemu zinazokumbwa na hali mbaya zaidi

    (GMT+08:00) 2017-06-24 18:25:22

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kufanya utafiti kuhusu kutatua suala la umaskini katika sehemu zinazokumbwa na hali mbaya zaidi ya tatizo hilo.

    Rais Xi Jinping amesema hayo katika kongamano lililofanyika wakati alipofanya ukaguzi mkoani Shanxi. Katika kongamano hilo alitoa hotuba muhimu akieleza kuwa, tangu mkutano mkuu wa 18 wa chama cha kikomunisti cha China ulipofanyika, kamati kuu imeliweka kuondoa umaskini kuwa alama ya kujenga jamii yenye maisha bora, ambapo kazi ya kupambana na umaskini kwa pande zote imeanzishwa kote nchini, hadi sasa mipango mbalimbali ya kamati kuu ya chama imetekelezwa vizuri, na kiwango cha maisha ya wananchi maskini kimeinuka kwa udhahiri.

    Pia amesisitiza kuwa kamati ya chama katika ngazi mbalimbali zinapaswa kufahamu kwa kina ugumu, umuhimu wa kazi ya kuondoa umaskini kwa muda uliopangwa, ili kuhakikisha sehemu na watu wanaokumbwa na hali mbaya zaidi ya umaskini kuingia katika jamii yenye maisha bora kwa pamoja na wananchi wote nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako