• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Syria imewaachia huru wafungwa 672

    (GMT+08:00) 2017-06-25 17:58:49

    Serikali ya Syria jana ilitangaza kuwa, ili kuhimiza mchakato wa maafikiano ya kitaifa, imewaachia huru wasyria 672 waliofungwa gerezani.

    Habari kutoka shirika la habari la Syria zinasema, waziri wa sheria wa Syria Bw. Hisham al-Sha'ar siku hiyo huko Damascus, mji mkuu wa nchi hiyo alikutana na wafungwa watakaoachiliwa huru na kutoa hotuba, akisema kuwa wafungwa hao 672 wanatoka mikoa mbalimbali ya Syria, ambapo 588 wakiwemo wanawake 91 walifungwa katika jela iliyoko katikati ya Damascus.

    Bw. Sha'ar amesema lengo la hatua hiyo ni kuwatunza wananchi na kuhimiza maafikiano ya kitaifa, na kutoa fursa kwa wafungwa kurejea katika maisha ya kawaida.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako