• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watatu wafariki na wengine 30 kupotea baada ya boti ya utalii kuzama Colombia

    (GMT+08:00) 2017-06-26 09:17:22

    Watu watatu walifariki dunia na wengine 30 hawajulikani walipo baada ya boti moja ya utalii iliyokuwa na abiria 150 kupinduka jumapili nchini Colombia. Mkuu wa polisi nchini Colombia amesema ajali hiyo ilitokea kwenye bwawa la Penol-Guatape katika jimbo la Antioquia, kaskazini magharibi mwa nchi hiyo. Katibu wa serikali ya jimbo hilo Victoria Ramirez amesema operesheni ya ukoaji inayoshirikisha wizara ya mambo ya ndani, jeshi na polisi bado inaendelea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako