• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Ufaransa aahidi kupeleka Umoja wa mataifa muswada kuhusu mazingira mwezi Septemba

    (GMT+08:00) 2017-06-26 09:27:34

    Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameahidi kufikisha mswada wa mazingira kwa Umoja wa kimataifa mwezi Septemba. Mswada huo ulioandaliwa na wataalam wa sheria wa kimataifa, una lengo la kuweka mpango wa kimataifa wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Akiongea kwenye mkutano uliowakutanisha wageni wa heshima akiwemo aliyekuwa gavana wa jimbo California Arnold Schwarzenegger na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw Ban Ki-moon, Rais Macron ametoa mwito kwa umoja wa mataifa kuchukua hatua zaidi katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, na kusema "umoja wa mataifa ni jukwaa sahihi kwa hatua hiyo".

    Muswada huo una vipengele 26 ikiwa ni pamoja na vinavyohusu kanuni ya kulipia utoaji hewa chafu, hali ya mazingira mazuri, haki ya habari, na kanuni ya kutoingilia mambo ya ndani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako