• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uturuki yalaani matakwa ya nchi kadhaa kwa Qatar kuhusu kutatua msukosuko wake wa kidiplomasia

    (GMT+08:00) 2017-06-26 09:50:23

    Rais Recep Erdogan wa Uturuki amelaani matakwa yaliyotolewa na nchi za ghuba dhidi ya Qatar kuwa yanakiuka sheria za kimataifa.

    Rais Erdogan siku hiyo huko Istanbul amesema matakwa 13 yaliyotolewa kwa Qatar kuhusu kutatua msukosuko wa kidiplomasia yanakwenda kinyume na sheria za kimataifa. Akizungumzia nchi za ghuba kuitaka Qatar isitishe ujenzi wa kituo cha jeshi la Uturuki nchini humo, rais Erdogan amesisitiza kuwa hakuna haja ya kuruhusiwa na nchi yoyote kwa Uturuki kusaini makubaliano ya ushirikiano wa ulinzi na nchi nyingine.

    Mwanzoni mwa mwezi huu, Saudi Arabia, Umoaj wa Falme za kiarabu, Bahrain na Misri zilitangaza kukatisha uhusiano wa kibalozi na Qatar, na kuishutumu Qatar kuwa inaunga mkono ugaidi na kuharibu usalama wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako