• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea na juhudi za kuboresha uhusiano kati ya Pakistan na Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-06-26 10:10:37

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amepongeza juhudi za Pakistan na Afghanistan kuendeleza uhusiano kati yao, na kusisitiza kuwa China itaendelea na juhudu za kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo.

    Bw. Wang Yi amewambia rais Mamnoon Hussain wa Pakistan kuwa ziara yake nchini Afghanistan na Pakistan inalenga kuhimiza maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

    Amesema taarifa ya pamoja iliyotolewa na China, Afghanistan na Pakistan inaonyesha dhamira ya Pakistan na Afghanistan kuboresha uhusiano kati yao na kujenga uaminifu, ikiwa ni ishara nzuri ya nchi hizo mbili kwa dunia nzima.

    Rais Hussain amesema kuboresha uhusiano kati ya Pakistan na Afghanistan si kama tu kuna maslahi kwa nchi hizo mbili, bali pia kunasaidia amani, utulivu na maendeleo ya kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako