• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mfuko wa maendeleo wa China na Afrika umekuwa njia muhimu kwa viwanda vya China kuwekeza barani Afrika

    (GMT+08:00) 2017-06-26 17:36:39

    Leo tarehe 26 Juni ni siku ya maadhimisho ya miaka 10 tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa maendeleo wa China na Afrika. Mwenyekiti wa bodi ya mfuko huo Bw. Chi Jianxin alipohojiwa na mwandishi wa habari wa Radio China Kimataifa alisema, ukiwa mfuko wa kwanza wa hisa wa China unaoshughulikia uwekezaji barani Afrika, mfuko huo siku zote unahimiza na kuunga mkono uwekezaji wa viwanda vya China barani Afrika.

    Mfuko wa maendeleo wa China na Afrika ulioanza kufanya kazi tarehe Juni mwaka 2007, ni njia muhimu kwa serikali ya China kufanya ushirikiano wenye ufanisi na Afrika. Mfuko huo unaoendeshwa na Benki ya maendeleo ya China ulipangwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 5. Mwezi Desemba mwaka 2015, Rais Xi Jinping wa China alitangaza katika mkutano wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika huko Johannesburg kuwa, China itaongeza dola za kimarekani bilioni 5 kwa ajili ya mfuko wa maendeleo kati ya China na Afrika, ambapo thamani ya mfuko huo iliongezeka na kufikia dola za kimarekani bilioni 10.

    Kutokana na msaada wa mfuko huo, katika miaka 10 iliyopita, viwanda vya China vilipiga hatua kwa kasi kuingia barani Afrika, na kuhimiza maendeleo ya uchumi na jamii na kuwanufaisha wenyeji wa huko. Mwenyeji wa bodi ya Mfuko wa maendeleo wa China na Afrika Bw. Chi Jianxin ameeleza kuwa, mfuko huo unatofautiana na misaada na mikopo isiyo na riba, unashughulikia uwekezaji barani Afrika, ili kuleta faida za uchumi na jamii. Bw. Chi Jianxin anasema:

    "Mfuko wa maendeleo wa China na Afrika unatafuta miradi yenye uwezo wa kupata maendeleo endelevu, na kuleta faida za uchumi kwa viwanda vyenyewe. Uwekezaji wa mfuko huo hautaleta mizigo yoyote ya madeni kwa sehemu zinazowekezwa, lakini faida zinazoletwa navyo zitaonekana katika sehemu hizo. Viwanda hivi vitachangia utoaji wa nafasi za ajira, mapato ya kodi, , na vitahimiza maendeleo endelevu ya uchumi wa huko."

    Takwimu zimeonesha kuwa, tangu kuanzishwa kwa mfuko huo, umefanya majadiliano na ushirikiano na viwanda zaidi ya 1,000, kufanya utafiti kuhusu miradi zaidi ya 500, na kuamua kufanya uwekezaji katika miradi 90 yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 4.3 katika nchi 36 barani Afrika. Miradi hiyo pia itahimiza viwanda vya China kuongeza uwekezaji kwa dola za kimarekani bilioni 20 barani Afrika, sekta za uwekezaji zitahusu ujenzi wa miundo mbinu, ushirikiano wa nishati, mambo ya kilimo na maisha ya wananchi, pamoja na uendelezaji wa maliasili.

    Misri ni moja kati ya nchi zilizoko katika "Ukanda mmoja, Njia moja." Mwaka 2013, mfuko wa maendeleo wa China na Afrika na kampuni ya Fengshang ya mkoa wa Jiangsu ambayo inaongoza kampuni nyingine katika vifaa na teknolojia za uzalishaji wa malisho, zilijenga kampuni ya hisa ya viwanda ya MIsri katika Eneo la ushirikiano wa uchumi na biashara kati ya China na Misri lililoko katika Ghuba ya Suez, na kupanua soko lake barani Afrika, ili kuhakikisha mahitaji ya usalama wa kilimo na maisha ya wananchi ya huko. Meneja mkuu wa kampuni hiyo Bw. Li Xiang Dong anasema:

    "Ushirikiano kati ya kampuni yetu na mfuko wa maendeleo ya China na Afrika unahusisha sekta mbili ikiwemo vifaa vya kutengeneza malisho, pamoja na maghala ya chakula. Nchi za Afrika ziko nyuma kiuchumi, na katika baadhi ya nchi, usalama wa chakula ni eneo la mkakati wa taifa. Ndiyo maana kutokana na mustakabali wa maendeleo ya Afrika, tuna imani juu ya mustakabali wa viwanda vya mashine ya kutengeneza malisho na maghala ya chakula."

    Kwa maoni ya mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa maendeleo wa China na Afrika Bw. Chi Jianxin, ana amini kuwa kutokana na ushirikiano wa kimataifa wa "Ukanda mmoja, Njia moja", mfuko wa maendeleo wa China na Afrika utaonesha umuhimu mkubwa zaidi. Akisema:

    "Pendekezo hilo linakaribisha ushiriki wa nchi zote duniani, na ushirikiano kati ya China na Afrika utanufaishwa kutokana na pendekezo hilo, ambapo maendeleo ya "Ukanda mmoja, Njia moja" yatahimiza bidhaa zinazotengenezwa na nchi za Afrika kuuzwa katika nchi zilizoko kwenye "ukanda mmoja, Njia moja", wakati huo huo maendeleo ya "Ukanda mmoja, Njia moja" pia yatahimiza kupanua soko la nchi za Afrika."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako