• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya waziri wa mambo ya nje wa China katika nchi za Afghanistan na Pakistan yapata mafanikio

    (GMT+08:00) 2017-06-26 19:17:11

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, ziara ya waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi katika nchi za Afghanistan na Pakistan mwishoni mwa wiki iliyopita imepata mafanikio makubwa.

    Geng amesema, katika ziara hiyo, Afghanistan na Pakistan zimeonesha urafiki wa dhati na kupiga hatua katika kuboresha uhusiano kati ya pande hizo mbili. Amesema, ziara ya Bw. Wang imetimiza makubaliano muhimu yaliyofikiwa kati ya viongozi wa China, Afghanistan na Pakistan, ili kusukuma mbele maendeleo mapya katika uhusiano kati ya China na Afghanistan na China na Pakistan. Katika ziara yake, Bw. Wang amesikiliza maoni ya viongozi wa nchi hizo kuhusu suala kati ya pande hizo mbili, na kusaidia kuboresha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na kuhimiza mchakato wa makubaliano ya amani nchini Afghanistan.

    Bw. Geng amesisitiza tena kuwa China haitaingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine, pia haitalazimisha nchi nyingine kufuata nia yake, lakini China inapenda kuzisaidia nchi za kirafiki zinapohitaji msaada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako