• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanane wauawa katika operesheni ya kuwasaka wapiganaji iliyofanywa na jeshi la Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-06-26 19:18:02

    Wizara ya ulinzi ya Afghanistan imesema, wapiganaji wanane wameuawa na wengine watano wamejeruhiwa wakati operesheni iliyofanywa na jeshi la nchi hiyo katika mikoa miwili inayokumbwa na vurugu.

    Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema wapiganajiwa kundi la Taliban wameuawa katika operesheni zilizofanywa kwenye mikoa ya Uruzgan na Wardak, ambapo pia gari la jeshi lililochukuliwa na wapiganaji hao limepatikana katika operesheni hiyo.

    Taarifa hiyo pia imesema askari wa jeshi la Afghanistan pia waliondoa mabomu na kutegua mabomu yaliyotegwa ardhini na kukamata silaha na risasi.

    Kundi la Taliban halijatoa tamko lolote kuhusiana na taarifa hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako