• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na waziri mkuu wa Sweden

    (GMT+08:00) 2017-06-26 19:19:36

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na waziri mkuu wa Sweden Bw. Stefan Lofven hapa Beijing.

    Rais Xi amemkaribisha Bw. Lofven kuhudhuria mkutano wa baraza la Davos la majira ya joto utakaofanyika hapa China. Rais Xi amesema, Sweden ni nchi ya kwanza ya magharibi iliyoanzisha uhusiano wa kibalozi na China. Kujenga uhusiano wa kiafya, utulivu na endelevu kati ya nchi hizo mbili sio tu kunaendana na maslahi ya nchi hizo, bali pia kunasaidia kuhimiza ushirikiano kati ya China na Ulaya ya Kaskazini na maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ulaya.

    Rais Xi pia amesema, China inasifia Sweden kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja, na kutaka pande mbili kuheshimu mfumo wa upande mwigine na njia ya kujiendeleza na kulinda maslahi ya kiini ya upande mwingine na ufuatiliaji mkubwa.

    Bw. Lofven ametoa salamu za pole kwa walioathiriwa na maporomoko ya ardhi yaliyotokea Jumamosi wilayani Mao, mkoani Sichuan. Pia amesema, Sweden inatilia maanani ushawishi wa China katika mambo ya kikanda na ya kimataifa, pia inazingatia ushirikiano na China chini ya utaratibu wa pande mbalimbali wa Umoja wa Mataifa.

    Habari nyingine zinasema, rais Xi leo pia amekutana na waziri mkuu wa Finland Bw Juha, Sipila.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako