• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Mauzo ya nje ya karafuu kushuka chini kwa asilimia 52: Zanzibar

    (GMT+08:00) 2017-06-26 20:00:58

    Kupungua kwa kiasi cha mauzo ya nje ya karafuu na kushuka kwa bei ya bidhaa hii katika soko la dunia imeathiri mauzo ya nje ya bidhaa Zanzibar ambayo imeshuka kwa asilimia 52.4 katiika mwisho wa mwaka mwezi Aprili 2017.

    Kulingana na Benki ya Tanzania, mapitio ya fedha ya kila mwezi, mwezi Mei 2017 , mauzo ya bidhaa yalipungua kutoka dola milioni 67.5 katika mwaka ulioisha Aprili 2016 hadi dola milioni 32.1 mwaka huu hadi mwezi.

    Thamani ya mauzo ya karafuu ilifikia dola milioni 17.0 chini kutoka dola milioni 45.7 kwa kipindi kama hicho mwaka 2016.

    Kuanguka kulihusishwa na kupungua kwa kiasi cha bidhaa na kushuka kwa bei, hii ni kulingana Ripoti ya Benki ya Tanzania BoT.

    Bei ilianguka kutoka dola 8,064 kwa tani hadi dola 7,750 kwa tani wakati kiasi cha mauzo ya nje kilipungua kutoka tani 5700 hadi tani 2200 katika kipindi hicho.

    Hali hiyo pia imeathiri utendaji wa jumla wa mauzo ya nje kama jumla ya bidhaa na mauzo ya nje ilipungua kutoka dola milioni 197.6 milioni awali hadi dola milioni 178.4 mwaka huu hadi Aprili 2017.

    Zanzibar inakabiliwa na changamoto ya ulaghai lakini serikali inasema inaongeza juhudi za kukomesha hali hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako