• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Sekta binafsi ya Uganda imeanza kuangalia bandari ya Dar es Salaam uchunguzi mkuu wa Kenya ukikaribia

    (GMT+08:00) 2017-06-26 20:01:37

    Ikiwa ni wiki sita zilizobakia Wakenya kwenda kwenye uchaguzi mkuu, Sekta binafsi ya Uganda imeanza kuangalia bandari ya Dar es Salaam kama njia mbadala ya kuagiza na kusafirisha bidhaa.

    Bandari ya Mombasa, ambayo kwa mujibu wa ripoti za hivi karibuni, imeandikisha ukuaji wa mizigo asilimia 11 katika robo ya kwanza ya 2017, inatumikia na Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan Kusini na DR Congo.

    Lakini kupitia uchanguzi unaosubiriwa bandari ya Mombasa inaonekana kukosa wateja, wengi wakihofia uwezekano wa machafuko ya uchanguzi.

    Wafanyibiashara wengi wangependelea sana kutumia bandari ya Mombasa, lakini uharibifu wa vitu baada ya uchaguzi wa 2007/8 uliathiri vibaya uchumi wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako