Rais Xi Jinping wa China amesifu utaratibu wa "Nchi moja, Mifumo Miwili" kuwa ni mpangilio bora zaidi wa kitaasisi katika kudumisha ustawi wa muda mrefu na utulivu wa Hong Kong.
Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, amesema hayo alipotembelea maonyesho yaliyofanyika kwenye Jumba la Taifa la Makumbusho hapa Beijing. Rais Xi pia amesifu mafanikio yaliyopatikana Hong Kong katika miaka 20 iliyopita.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |