• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China iko tayari kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kati ya viongozi wa China na Rwanda

    (GMT+08:00) 2017-06-27 09:27:36

     

    Mjumbe maalum wa serikali ya China Bw Xi Jinghu amesema China iko tayari kufanya kazi kwa karibu na Rwanda ili kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa pande mbili.

    Akiongea mjini Kigali baada ya kukutana na Rais Paul Kagame wa Rwanda, Bw Xu amesema tangu China na Rwanda zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 46 iliyopita, uhusiano kati ya pande hizo mbili umekuwa ukiendelea vizuri.

    Rais Kagame amesema kwenye mkutano huo kuwa, baada ya ziara aliyofanya nchini China mwezi Machi na kufikia makubaliano ya ushirikiano na Rais Xi Jinping, uhusiano kati ya pande mbili una mwelekeo mzuri. Amesema Rwanda inathamini sana uhusiano huo, na iko tayari kuimarisha ushirikiano na China kwenye ujenzi wa maendeleo ya viwanda, utafiti wa nishati, ujenzi wa miundo mbinu, utalii na kilimo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako