• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa kilele wa 29 wa AU kuanza Addis Ababa

    (GMT+08:00) 2017-06-27 09:29:49

    Mkutano wa Kilele wa 29 wa Umoja wa Afrika unatarajiwa kuanza leo na kuendelea hadi Julai 4 kwenye makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa.

    Mkutano huo unaendeshwa chini ya kauli mbiu ya uwekezaji kwa vijana. Katika taarifa yake AU imesema mkutano wa 34 wa Kamati ya Wawakilishi wa Kudumu, pia utafanyika katika siku mbili za mwanzo za mkutano wa kilele. Kamati hiyo inatarajiwa kuandaa ajenda ya mkutano mkuu wa kilele kwa kutoa mapendekezo yanayofaa ya kuzingatiwa na baraza tendaji, ambalo limepangwa kufanyika kuanzia Juni 30 hadi Julai mosi.

    Mkutano wa Kamati ya wawakilishi utawaleta pamoja mabalozi wote wa nchi 55 wanachama wa AU pamoja na maofisa wengine wakuu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako