• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kichinjio cha tatu nchini Kenya cha punda chafunguliwa Turkana

    (GMT+08:00) 2017-06-27 09:44:04

    Kichinjio cha tatu cha punda nchini Kenya kimefunguliwa jana katika eneo la Nakwaalele mjini Lodwar,katika kaunti ya Turkana. Kichinjio cha kampuni ya Zilzha kutoka China kitasindika nyama ya punda pamoja na ngozi kwa ajili ya usafirishaji hadi China na nchi nyengine za mashariki ya mbali.

    Kichinjio hiki kilichofunguliwa Turkana kitashindana na vichinjio vingine viwili ambavyo vlifunguliwa na vinafanya kazi;kimoja kinapatikana Maraigushu,mjini Naivasha katika kaunti ya Nakuru,na kingine katika eneo la Mogotio katika kaunti ya Baringo.

    Xu Jing Long,mmojawapo wa wachina wanaoendesha kichinjio cha Zilzha cha Turkana amesema kichinjio hicho kitatoa ajira kwa wenyeji zaidi ya 200.Aidha Long alisema hamu yao hasa ipo katika ngozi ya punda ambayo ina soko kubwa nchini China.

    Ngozi ya punda huchemshwa na baadae hutumika kutengeza dawa ya kiasili ya China ijulikanayo kama 'Ejiao' .Ejiao inatumika kutibu upungufu wa damu,kikohozi sugu,kukosa usingizi na magonjwa mengineyo.

    Xu Jing Long amesema nyama na bidhaa za punda zitakazotoka katika kichinjio hicho zitasafirishwa hadi nchini China na hazitauzwa katika soko la Kenya.

    'Mradi huu mkubwa ni kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi pekee.Tuna soko nchini China.Kwa hivyo haifai kuwa na wasiwasi wowote'

    Afisa wa Afya kutoka Wizara ya Mifugo nchini Kenya Dkt Jonathan Tanui ndiye anayesimamia shughuli za uchinjaji katika kichinjio cha Zilzha.

    'Nimekuwa katika shirika la nyama nchini Kenya,vichinjio vya Dagoretti,Burma,na vichinjio vingine nchini-Naweza kuthibitisha kuwa kichinjio hiki kimeafikia viwango vinavyohitajika.'

    Anasema kuwa wanyama hao kabla ya kuchinjwa ni lazima wapimwe ili kuhakikisha kuwa ni salama kwa kuliwa.

    'Lazima tuwakague na kuwapima mmoja baada ya mwingine ili kuhakikisha kuwa hawana maradhi kama vile tetanus,rabies au magonjwa mengine ambayo yanaweza kuathiri binadamu.Licha ya kuwa Punda amethibishwa kuwa salama kwa chakula lakini nchini Kenya bado watu wengi hawajakumbatia ulaji wa nyama hiyo'

    Kichinjio hiki kimetoa ajira kwa watu zaidi ya 200 huku famila nyingi zikijikimu kupitia kichinjio hiki.

    Punda mmoja anauzwa katika ya shilingi 8,000 hadi 10,000. Nyama inayotoka katika kichinjio hiki husafirishwa China na nchi nyingine za bara Asia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako