• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Iraq latwaa maeneo mawili ya makazi katika mji mkongwe magharibi mwa Mosul

    (GMT+08:00) 2017-06-27 09:49:34

    Jeshi la Iraq limekomboa maeneo mawili ya makazi ya al-Farouq al-Oula kutoka kwa wapiganaji wa kundi la IS baada ya kupambana vikali na kundi hilo, wakati linaendelea kusonga mbele kuelekea katikati ya mji mkongwe magharibi mwa Mosul.

    Kwa mujibu wa jeshi la Iraq, hivi sasa ni asilimia 1 tu ya mji wa Mosul bado inadhibitiwa na wapiganaji wa kundi la IS, na vikosi vya Iraq vinasonga mbele kutoka pande zote.

    Ripoti ya Umoja wa mataifa inasema raia wapatao laki moja bado wamekwama kwenye maeneo ya katikati yanayodhibitiwa na kundi la IS katika mji mkongwe wa Mosul, ambao wanatumiwa na wapiganaji wa kundi hilo kama ngao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako