• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bw Guterres atoa wito wa kupambana na matumizi na usafirishaji wa dawa za kulevya

    (GMT+08:00) 2017-06-27 10:00:43

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw António Guterres ametoa mwito kwa serikali za nchi zote zitekeleze ahadi zilizotoa mwaka jana na kuchukua hatua zenye uratibu na uwiano kwa pande zote, ili kutafuta njia endelevu ya kupambana na dawa za kulevya.

    Bw Guterres amesema kwamba mkutano maalumu wa pamoja kuhusu dawa za kulevya uliofanyika mjini New York mwezi Aprili mwaka jana una maana kubwa ya kuweka mpango makini kwa kazi za siku za baadaye. Nchi zote zinatakiwa kufanya juhudi katika kupambana na matumizi na uuzaji wa dawa za kulevya, na kuhakikisha kampeni dhidi ya dawa za kulevya zinahimiza usawa, haki za binadamu na maendeleo endelevu, na kusaidia amani na usalama.

    Katika miaka mitano iliyopita, China imeshughulikia kesi laki 7.24 zinazohusu dawa za kulevya, na kuwakamata watuhumiwa laki 5.34 na tani 370 za dawa za kulevya. Na watu milioni 1.45 wanaotumia dawa za kulevya wamepata matibabu nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako