• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya waitaka Uingereza kutoa mpango bayana wa Brexit

    (GMT+08:00) 2017-06-27 10:14:02

    Mjumbe wa kamati ya Umoja wa Ulaya anayeshughulikia mazungumzo ya Brexit Bw Michel Barnier ameitaka serikali ya Uingereza kutoa mpango wazi wa kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

    Bw. Barnier amesema lengo la Umoja wa Ulaya la kulinda haki za raia wake ni usawa wa ulinzi kwa wote chini ya sheria za Umoja wa Ulaya, na Uingereza inatakiwa kutoa mpango bayana na wa uhakika zaidi.

    Na jana waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May alitangaza mpango wenye vipengele tisa kuhusu haki za raia zaidi milioni 3 wa Umoja wa Ulaya watakaoendelea kuishi nchini Uingereza baada ya Brexit.

    Amesema kutokana na mpango huo hakuna mtu atakayelazimishwa kuondoka baada ya Uingereza kumaliza uanachama wake wa Umoja wa Ulaya ndani ya miaka miwili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako