• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Marekani ahimiza India iipunguzie nchi hiyo vikwazo vya biashara

    (GMT+08:00) 2017-06-27 17:46:26

    Rais Donald Trump wa Marekani amekutana na kufanya mazungumzo na waziri mkuu wa India Bw. Narendra Modi aliyeko nchini Marekani.

    Katika mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye ikulu ya Marekani, viongozi hao wamejadiliana masuala kuhusu biashara na usalama, huku rais Trump akiitaka serikali ya India ipunguze vikwazo vya biashara kwa Marekani.

    Rais Trump amezitaka nchi hizo mbili ziunde uhusiano wa kibiashara wa usawa na kunufaishana, na kusema India inapaswa kupunguza vikwazo vilivyowekwa dhidi ya bidhaa za Marekani kuingia kwenye soko la India ili kupunguza ufinyu wa biashara wa Marekani kwa India.

    Kutokana na kukua kwa uchumi wa India, Marekani inataka kuuza nishati zaidi nchini India. Pia rais Trump amesema, hivi sasa nchi hizo mbili zinafanya majadiliano kuhusu mkataba wa kununua gesi kutoka Marekani kwa India.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako