• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yasema huenda Syria inajiandaa kufanya shambulizi la silaha za kikemikali

    (GMT+08:00) 2017-06-27 19:12:42

    Marekani imesema huenda serikali ya Syria inafanya maandalizi ya shambulizi lingine la kikemikali, na kuonya kuwa, kama shambulizi hilo litafanywa, Syria itapata hasara kubwa.

    Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani imesema, vitendo vinavyofanywa na serikali ya Syria ni sawa na maandalizi yaliyofanywa na serikali hiyo kabla ya shambulizi la silaha za kikemikali lililotokea Aprili 4 mwaka huu.

    Hata hivyo serikali ya Syria imekanusha lawama hizo, na kusema tuhuma hizo za Marekani ni uchokozi wa wazi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako