• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asisitiza kuwa utoaji wa nafasi za ajira ni msingi wa kuhakikisha ongezeko la uchumi shirikishi

    (GMT+08:00) 2017-06-27 19:13:19

    Mkutano wa Baraza la uchumi duniani la mwaka 2017 ambalo linajulikana kama "Baraza la Davos la majira ya joto" umefunguliwa leo mjini Dalian, China. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni "kutimiza ongezeko la uchumi shirikishi katika hatua ya Mapinduzi ya nne ya viwanda."

    Hii ni mara ya tano mfululizo kwa waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang kushiriki katika ufunguzi wa mkutano wa Baraza la Davos la Majira ya Joto tangu mwaka 2013, na kutoa hotuba katika ufunguzi huo. Katika hotuba aliyoyatoa leo, Bw. Li Keqiang amefafanua umuhimu wa kuhimiza ongezeko la uchumi shirikishi chini ya hali ya kufufuka kwa uchumi duniani ambayo bado si ya kudumu, na hatua zilizochukuliwa na China katika ongezeko hilo.

    Bw. Li Keqiang amesema, duru mpya ya mapinduzi ya viwanda inayohusisha mambo ya mtandao wa Internet, digitali na akili Intelligent, si kama tu imeleta mahitaji mapya na nafasi mpya za utoaji wa huduma, bali pia imeziletea pande mbalimbali fursa nyingi za kushiriki katika mapinduzi hayo kwa usawa. Na kuna uwezekano mkubwa zaidi kutimiza ongezeko shirikishi katika duru mpya ya mapinduzi haya. Bw. Li anasema:

    "Hivi sasa bidhaa zenye umaalumu wa kipekee za mazao zinazotengenezwa na wakulima wanaoishi milimani, zinaweza kuuzwa katika miji mikubwa nchini China kwa njia mbalimbali za uchukuzi, na bei ni mara kadhaa kuliko zile zinazozwa katika sehemu zinakotoka. Hali hii inaonesha kuwa, endapo tunatoa fursa ya kutosha kwa watu wote ambao wana uwezo na nia ya kufanya matengenezo watapata fursa kubwa ambazo hawakutarajia."

    Bw. Li Keqiang pia amesema, China imechukua hatua mbalimbali za kuhimiza ongezeko shirikishi, na katika miaka kadhaa iliyopita, nafasi mpya zilizoongezeka kila mwaka nchini China zilizidi milioni 13, na kiwango cha kupotea ajira kimedumisha chini ya asilimia 5. Bw. Li anasema:

    "Kwanza tunapaswa kutoa kipaumbele katika kutoa nafasi za ajira, kwani ajira ni msingi wa kuhakikisha ongezeko la uchumi shirikishi. Hivyo tunachukua hatua mbalimbali za kuhimiza utoaji wa nafasi za ajira, ili kuhakikisha kila familia ina mtu zaidi ya mmoja mwenye ajira ya kudumu."

    Katika miaka ya hivi karibuni, kuanzisha biashara na kufanya uvumbuzi umekuwa ni umaalumu mkubwa wa maendeleo ya uchumi wa China. Takwimu zimeonesha kuwa, China imeshika nafasi ya 22 kati ya nchi zinazofanya uvumbuzi duniani, na nafasi hiyo inaongoza nchi nyingine zinaoendelea duniani. Mwenyekiti wa Baraza la uchumi duniani WEF Bw. Klaus Schwab anasema:

    "China imetimiza ongezeko la asilimia 7 la uchumi, hayo ni mafanikio makubwa sana. Serikali ya China ni serikali inayotekeleza vizuri kuyahusisha mapinduzi ya nne ya viwanda kwenye sera zake."

    Wajumbe zaidi ya 2,000 wakiwemo viongozi wa nchi, maofisa, wanaviwanda, wataalamu na waandishi wa habari kutoka nchi zaidi ya 90 walihudhuria ufunguzi wa mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako