• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi ya vifo kutokana na ajali ya moto wa lori la mafuta nchini Pakistan yafikia 158

    (GMT+08:00) 2017-06-28 09:07:49

    Idadi ya vifo vya watu kutokana na ajali ya moto wa lori la mafuta lililopinduka jumapili kwenye eneo la Bahawalpur mkoani Punjab, mashariki mwa Pakistan imeongezeka na kufikia 158, baada ya majeruhi 18 walioungua vibaya kufariki dunia wakipewa matibabu. Ofisa wa serikali ya mkoa huo amesema idadi ya vifo huenda ikaongezeka kutokana na majeruhi wengine 22 kuwa katika hali mahututi. Waziri mkuu wa nchi hiyo Bw. Nawaz Sharif ameamuru kufanyika kwa uchunguzi kamili kuhusu janga hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako